Miili ya watu 10 hadi 20 iliyoungua moto kupatikana kila siku Hawaii

 

Vikosi vya ufuatiliaji wa maafa ya moto kwenye nyumba na magari yaliyoungua huko Hawaii, vinatarajia kupata miili 10 hadi 20 kila siku, Gavana wa jimbo hilo ametahadharisha.

Vifo vilivyotokana na moto huo hadi sasa vimefikia watu 90, na kufanya tukio hilo kuwa ni moja ya matukio mabaya ya moto wa nyika kuwahi kutokea kwa zaidi ya karne moja Marekani.

Gavana Josh Green ameiambia CBS News kwamba itachukua zaidi ya siku 10 kupata uhakika wa idadi ya vifo vya watu vilivyotokana na moto huo.

Idadi ya watu ambao hawajulikani walipo tangu kutokea kwa maafa ya moto huo wa nyika Hawaii imefikia watu 1,300.

Chapisha Maoni

0 Maoni