Varane aipatia ushindi wa bahati Manchester United

 

Raphael Varane amefunga goli dakika 14 kabla ya mpira kumalizika na kuipa ushindi wa bahati Manchester United dhidi ya Wolves katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Kikosi cha kocha Erik ten Hag kilitengeneza nafasi za kutafuta goli kwa shida hadi pale Bruno Frenandez alipompatia pande safi ndani ya boksi Aaron Wan-Bissaka.

Beki huyo wa kulia wa United alitulia na kunyanyua mpira kwenye eneo la goli ndipo Varane alipotumia urefu wake kuruka juu ya Nelson Semedo na kufunga goli la kichwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni