Wavuliwa nguo kiwandani kumsaka aliye kwenye hedhi

 

Watu watatu wamekamatwa, baada ya wafanyakazi wa kampuni ya kutengeneza jibini ya Kenya kudai wamelazimishwa kuvua nguo ili kumbaini ni nani yupo kwenye siku zake za hedhi.

Meneja wa Kampuni hiyo ya Brown’s Food Company, aliwakusanya wafanyakazi wanawake ili kubaini ni nani alitupa pedi katika pipa lisilosahihi, afisa mmoja amesema.

Meneja huyo aliwaagiza wafanyakazi wanawake kuvua nguo, baada ya jitihada zake za kumpata mwanamke aliyetupa pedi hiyo kimakosa kushindwa kuzaa matunda.

Kampuni ya Brown's imesema kwamba imemsimamisha kazi meneja wake huyo anayetuhumiwa kufanya udhalilishaji huo wa kijinsia, ili kupisha uchunguzi.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni