Vita mpya Elon Musk na Mark Zuckerberg

 

Vita ya manguli wa mitandao ya kijamjj nchini Marekani Elon Musk na Mark Zuckerberg imeendelea kuwa gumzo baada ya kila uchwao kubuni mbinu mbalimbali za kuwavutia wateja wao.


Kinachochagiza gumzo hilo ni Mtandao mpya wa Kijamii wa THREADS ambao unamilikiwa na Kampuni ya META ya Marekani inayomiliki Mitandao mingine kama Facebook, Instagram na WhatsApp, chini ya CEO Mark Zuckerberg.


Kwa sasa mtandao huo mpya uliozinduliwa siku chache zilizopita umefikisha Watumiaji zaidi milioni 30 kwenye siku yake ya kwanza ya kuzinduliwa.


Zuckerberg amekubaliana na wazo la kwamba application hiyo mpya  itakuwa Mpinzani namba moja wa mtandao wa Elon Musk wa Twitter huku wazo hilo likiwafanya Wakurugenzi Wakuu wa Makampuni hayo makubwa ya teknolojia kusema watawema pambano la ngumi. 



Kwa  upande wake Elon Musk amejibu uzinduzi wa mtandao huo mpya kupitia post kadhaa kwenye Twitter akisema "Kheri kushambuliwa na Watu usiowajua kwenye Twitter kuliko kujiingiza katika furaha ya uongo ya kujificha kupitia Instagram” 


Kwa mujibu wa Watendaji wamesema hakutakuwa na kikomo kwa idadi ya post ambazo Watumiaji wanaweza kuona kwenye threads na mtandao huo utapatikana kwenye zaidi ya nchi 100 kwa Watumiaji wa bidhaa za Apple na Google Play Store.


Threads ni Mtandao ambao unatazamiwa kuleta ushindani mkubwa sana kwa Mtandao wa Twitter ambao sasa upo chini ya Bilionea Ellon Musk ambapo Watumiaji wa Instagram ambao wako verified wamepewa upendeleo maalum wa kuwekewa tiki za bluu papohapo wanapojiunga na THREADS.

Chapisha Maoni

0 Maoni