Washirika kadhaa wa Marekani, wameonyesha kutoafikiana na uamuzi wa nchi hiyo kuipatia Ukraine mabomu ya aina ya cluster.
Ijumaa, Marekani ilithibitisha imepeleka silaha hiyo yenye
utata nchini Ukraine, huku Rais Joe Biden akiita hatua hiyo kuwa ni “uamuzi
mgumu mno”.
Kwa upande wa Uingereza, Canada, New Zealand na Hispania
wamepinga matumizi ya silaha hiyo.
Mabomu ya cluster yamepigwa marufuku katika zaidi ya nchi 100
kutokana na hatari kwa raia inayosababishwa
na mabomu hayo.
Mabomu hayo yanaporushwa husambaza mabomu madogo mithili ya
risasi yenye kuua hata watu wasio na hatia.
0 Maoni