Waasi wanaodaiwa kuwa ni wa M23 waua watu 11 DRC

Watu wapatao 11 wamekutwa wakiwa wamekufa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapo jana, ambapo vyanzo kutoka eneo la Rutshuru vimewatuhumu waasi wa M23 kwa mauaji hayo.

Mashuhuda wamesema miili ya watu imekutwa eneo la Bukombo, Kilomita 100 kaskazini mwa mji mkuu wa mkoa wa Goma baada ya waasi hao kuondoka kwenye eneo la tukio.

Moja ya taasisi isiyo ya kiserikali imesema waliokufa ni watu 12, ambapo waasi hao walipambana na kikundi cha jamii iliyokuwa ikijilinda, na waasi wameondoka na watu waliowalazimisha kubeba mizigo.

Chapisha Maoni

0 Maoni