Vyama 18 vyakitokeza kuomba usajili

 

Ikiwa ni mwaka mmoja umesalia kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa na miaka miwili kufanyika uchaguzi mkuu vyama vya siasa 18 vimejitokeza kuomba usajili.


Hayo yamebainishwa na Msajili  wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi amesema Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kikao kazi na viongozi wa vyama vya siasa nchini ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye uhakiki huo Mutungi amesema kwamba hawezi kusajili vyama vipya kabla ya kufanyika uhakiki katika vyama vilivyopo.


Kwa mujibu wa Jaji Mutungi amesema wanaotaka kufuta hati chafu ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa kuhakikisha vyama vinakuwa na wataalamu wa fedha ambao watakuwa wanafanya shughuli kwa kuzingatia weledi.


Shughuli ya uhakiki huo inatarajiwa kuanzia Julai 20 mwaka huu ambapo ofisi ya Msajili inawajibika kulinda uhai wa vyama hivyo kwa kuvikagua na kubainisha mapungufu yanayojitokeza kisha kutoa muda kwa utekelezaji.

Chapisha Maoni

0 Maoni