Mashabiki wafurika Messi akitambulishwa Inter Miami

 

Lionel Messi ametambulishwa rasmi mbele ya mashabiki wa Inter Miami kwenye dimba la DRV PNK nchini Marekani.

Tiketi zote za mauzo ya kumuona Messi zilimalizwa na mashabiki 20,000, waliovumilia mvua na radi ili kumuona mchezaji wao huyo mpya mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mara saba.

Akiongea kwa kifupi kwa lugha ya Kihispania, Messi, 36, amewashukuru mashabiki na kusema kuwa anamatumaini ya kufanya vyema ambayo daima huwanayo.

Mchezaji huyo raia wa Argentina aliyetwa kombe la dunia, amejiunga na klabu ya ligi ya Major League Soccer (MLS), hadi mwishoni mwa 2025.

Chapisha Maoni

0 Maoni