Rais Mstaafu Kenyatta amuonya Ruto, asema awaache Mama yake na Mtoto wake

 

Ikiwa hali ya kisiasa nchini Kenya imegubikwa na sintofahamu baada ya upinzani kuendelea kushinikiza mabadiliko na unafuu wa maisha Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta amelazimika kutoa ya moyoni.


Maswahibu yamemfika  Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kumlazimu kuzungumza huku akiitaka  Serikali ya Kenya inayoongozwa na Rais Ruto isimsumbue Mama yake na Watoto wake na kama inapanga kufanya kitu kibaya ifanye kwake. 


Kenyatta amesema hayo Julai 21 baada ya kutoka Ofisini kwake na kwenda nyumbani kwa Mtoto wake ambaye alimpa taarifa ya kuvamiwa na Watu waliojitambulisha ni kutoka Ofisi ya DCI wakiwa na gari lenye namba za usajili za Sudan, ikiwa zimepita siku chache tangu Walinzi wa Serikali waondolewe kwa Mama yake Kenyatta.

Kenyatta amesema “Hawa wamefika kwa Mtoto wangu wa kiume wanataka kumuona, aliponiambia nikawaambia Polisi wakitaka kufanya kitu hawaji na namba za gari za kigeni, wanatakiwa kuja na waranti na waseme wanakukamata kwa kosa gani, nikawaambia msifunge geti nikawahi hapa naambiwa wameondoka maana nilitaka kuwauliza mnafanya nini kwa Mwanangu"


"Naona haya yanaendelea mfululizo, kuna Walinzi walikuwa wanamlinda Mama yangu kwa miaka mingi juzi ulinzi umeondolewa tena usiku, sasa najiuliza Serikali inataka nini kama unanitaka Mimi, mnajua nilipo siku zote njooni”


Amenukuliwa akisema “Labda ukimya wakati mwingine sio sahihi, najiuliza kivipi nifadhili maandamo?, au kwasababu ya urafiki wangu na Odinga? siruhusiwi kuongea na Odinga?, kuna sheria Kenya inayosema kwamba ni kosa la jinai Mtu kuongea na Rafiki yake?, 


Kenyatta aliyeonekana na ghadhabu baada ya tukio hilo amezungumza kuhusu kufananjsha watu hao na magaidi na kusema “labda kama uniambie wao ni Magaidi wasiopaswa kuongea na Mtu? lakini Kenya ni Nchi ya Kidemokrasia, labda kuna kitu wanapanga kufanya wafanye kwangu Mama yangu na Mwanangu wanahusika nini?”

Chapisha Maoni

0 Maoni