Manchester United wakaribia kumnasa kipa Onana

 

Manchester United wanamatumaini ya kukamilisha dili la kumnasa kipa wa Inter Milan Andre Onana.

Kocha Erik ten Hag yupo makini katika kutatua tatizo la nafasi ya kipa Old Trafford, kutokana na uwezekano wa kumkosa kipa wao David de Gea.

Mkataba wa De Gea kukaa Old Trafford ulimalizika mwishoni mwa mwezi uliopita na bado hajapewa ofa ya kuongezewa mkataba mpya.

Onana, mwenye umri wa miaka 27 hajafungwa goli kwenye mechi nane kati michezo 24 ya ligi ya Italia ya Seria A aliyocheza msimu huu.

Chapisha Maoni

0 Maoni