Watanzania wachangamkia ofa ya Sabasaba kutalii Kilwa

 

Kundi la watalii wa ndani wapatao 21, wametumia kikamilifu ofa maalum ya Sabasaba kwenda kutalii katika Hifadhi ya Magofu ya kale Kilwa Kisiwani iliyo chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Ofa hii imelenga kuhamasisha Utalii wa ndani na kuwawezesha watanzania wote kutembelea hifadhi hiyo Kwa kupunguzo kubwa la gharama ambapo mtalii Kwa kulipia gharama ya Shillingi 130,000/= ataweza kutalii  baharini katika visiwa vya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara Kwa kutumia boti la Kisasa lenye kioo maalum chenye kumwezesha mtalii kuona mandhari na viumbe mbalimbali vilivyopo chini ya bahari Kwa siku mbili

Kupitia malipo ya kiasi hicho mtalii pia ataweza kupata   chakula, vinywaji na viburudisho mbalimbali

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inaendelea kuwahamasisha watanzania wote kutumia kipindi hiki cha maonesho ya Sabasaba kutembelea hifadhi zake zote nchini hususan Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kwani ni kipindi maalum chenye punguzo maalum Kwa watalii wa ndani

Na. Beatus Maganja

Chapisha Maoni

0 Maoni