Maandamano ya kuipinga serikali yaitikisa Kenya

 

Maandamano yakuipinga serikali ya Kenya yamekuwa yakiendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kupinga kupanda kwa gharama za maisha.

Maaandamano hayo yaliyoitishwa na chama cha Azimio leo yamepelekea kusita kwa baadhi ya shughuli katika maeneo mbalimbali za nchi hiyo.

Huko Nakuru polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji ambao wamechoma moto matairi barabarani na kuweka mawe.

Katika eneo la Mathare, Jijini Nairobi waandamanaji wamekuwa wakiwatupia mawe polisi wanaojaribu kuzima maandamano yao.

Waandamanaji wa huko Nyamira wao wamekuja na aina yao ya maandamano kwa kubeba sufuria tupu katika kuonyesha hawana chakula.

Nako Mombasa polisi wa usalama barabrani wamelazimika kukaa kando kupisha askari wa kudhibiti fujo kukabiliana na waandamanaji.

Chanzo: Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii Kenya

Chapisha Maoni

0 Maoni