Nchi 10 bora zinazoongoza kwa amani Afrika hizi hapa

Nchi ya Mauritius inaongoza kwa kuwa nchi yenye amani katika bara la Afrika ikishika nafasi ya kumi katika viwango vya mataifa yenye amani duniani.

Katika ripoti hiyo ya taasisi ya Uchumi na Amani (IEP), Sudan Kusini ndio nchi inayoshika mkia kwa kutokuwa na amani Afrika.

Katika miaka 15 iliyopita dunia imekuwa ikipoteza amani, ambapo viwango vya amani vimekuwa vikipungua kwa wastani wa asilimia 5.

Orodha ya nchi kumi bora kwa amani Afrika ni Mauritius, Botswana, Sierra Leone, Ghana, Senegal, Madagascar, Namibia, Gambia, Zambia na Liberia.

Chapisha Maoni

0 Maoni