Wosia halali wa mwanamuziki Aretha Franklin ni wa 2014

 

Mahakama ya Michigan imetoa uamuzi kuhusu nyaraka za mwaka 2014, zilizopatikana kwenye kochi la mwanamuziki Aretha Franklin baada ya kifo chake, kuwa ni wosia halali wa mabilioni ya dola ya mali zake.

Shauri hilo lililotolewa uamuzi wake kwa siku mbili, limetokana na watoto wa Malkia huyo wa muziki wa Soul, kugombania uhalali wa nyaraka mbili zilizoandikwa kwa mkono kuwa ndio wosia wake wa mwisho.

Mwanasheria wa watoto wawili wa kiume wa Franklin, amesema kwamba ndugu yao wa kambo, alikuwa anataka ndugu zake hao wawili wasirithi mali za mama yao Aretha Franklin.

Hukumu hiyo iliyotolewa Jumanne, imemaliza karibu miaka mitano ya malumbano ya kisheria Mahakamani ya familia hiyo ya mwanamuziki Aretha Franklin.

Chapisha Maoni

0 Maoni