CCM haiwezi kuiuza nchi, watakaouza nchi ni makuwadi wa mabeberu- Wasira

 

Mwanasiasa mkongwe Stephen Wasira amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakiwezi kuiuza nchi, wala hakuna kiongozi anayetoka ndani ya CCM atakayeiuza nchi kama inavyodaiwa na wanaopinga uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam na kampuni ya DP World.

Akiongea leo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Mtwara, kabla ya kuongea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo, Wasira amesema watakaouza nchi ni madalali na makuwadi wa mabeberu na wala si CCM.

“Mimi nilishiriki katika kudai uhuru wa nchi hii, nikiwa na umri wa miaka 15 natoka shule naenda kuimba na kumtukana mkoloni ili akasirike aondoke, siwezi kushuhudia nchi hii inauzwa nikakaa kimya,” amesema Wassira na kuongeza “Chama cha CCM hakiwezi kuiuza nchi na wala hawezi kutokea kiongozi wa CCM atakayeuza nchi kwa saba sisi tunadhamana tuliyoridhi kutoka kwa TANU na Afro Shirazi.

Kuhusu madai ya kuwa usalama wa bandari kuachiwa wageni, Wasira amesema usalama wa bandari na bandari kama mpaka utabakia chini ya vyombo vya ulinzi na usalama, na wala hakuna mgeni atakayeachiwa kulinda bandari.

Chapisha Maoni

0 Maoni