Rais Samia alia na wanawake mmomonyoko wa maadili


Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake kujifanyia tathmini ili kuona namna ya kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili nchini ikiwemo kushikamana na kulea jamii.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 16, 2023 alipohutubia katika Kongamano la Wanawake wa Kiislam kuelekea maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1445 Hijiria.


Amesema kila mwanamke ana wajibu wa kusimamia maadili na kuwa ana mchango mkubwa katika kujenga au kumomonyoa madili ya familia kwa ujumla.


Aidha amewataka wanawake kujiepusha na vitendo vya unyanyasaji kwakuwa vinarejesha nyuma maendeleo ya kiuchumi,kisiasa na kijamii.



Kwa upande wa fursa amewataka wanawake kujiendeleza kielimu na kujitokeza kutumia fursa za kimaisha kila zinapojitokeza ili waweze kuinusuru jamii kwa kupambana na changamoto zinazojitokeza.


Katika kurekebisha maadili yaliyomomonyoka, tuangalie fursa zetu ni zipi, tunaweza kufanya nini, fursa ya kwanza walimu wazuri tunao, Serikali inatuunga mkono, wengi wanajitokeza kutoa mihadhara kuwawezesha wengine,” amesema.
Baada ya kuangalia fursa, amesema eneo lingine wanalopaswa kujua ni vikwazo vya kuyafikia hayo wanayoyatarajia.

“Unakuta wifi yako ana kazi nzuri anatoka anakwenda kufanya kazi, unakwenda kwake usipomkuta unasema mwanamke gani hatulii nyumbani, hivi ndivyo vikwazo vyenyewe,” amesema.

Chapisha Maoni

0 Maoni