Ashambulia na kuua watoto wa Chekeche kwa kisu

 

Watu sita, wakiwamo watoto watatu wameuawa kwa kuchomwa na kisu leo asubuhi kwenye shule ya Chekechea katika mkoa wa kusini mwa China wa Guangdong.

Polisi wamesema kwamba wamemkamata kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 25, ambaye jina lake la ukoo ni Wu kwenye mji wa Lianjiang.

Wengine waliouwa katika tukio hilo ni mwalimu na wazazi wawili, shirika la habari la AFP, limevinukuu vyombo vya habari vya China. Mtu mmoja pia amejeruhiwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni