Waokoaji wa Hispania wanatafuta boti lililotoweka likiwa na
wahamiaji 200 wa Afrika, ambao wametoweka kwa zaidi ya wiki kwenye eneo la kisiwa
cha Canary.
Waokoaji hao wa kundi la Walking Borders, wamesema boti hiyo
ilikuwa inatokea Kafountine, mji wa pwani ya kusini mwa Senegal umbali wa
kilomita 1,700, kutoka Tenerife.
Kundi hilo limesema kwamba watoto wengi walikuwamo kwenye
boti hiyo, ambapo pia boti nyingine mbili za wahamiaji wa Afrika zimeripotiwa
nazo kutoweka majini.
0 Maoni