Mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 19, aliyeibua utata
iwapo alipata alama za juu za ufaulu kwenye mtiahani wa taifa, amekiri kuwa
alighushi matokeo ya mtihani wa taifa wa mwaka huu.
Mgogoro wa matokeo ya mwanafunzi huyo Ejikeme Joy Mmesoma
ulitinga kwenye Bunge la Nigeria, ambapo wabunge walilazimika kujadili suala la
matokeo ya mwanafunzi huyo.
Ejikeme Joy Mmesoma amejikuta akipongezwa tangu alipojitokeza
na kutangaza amepata ufaulu wa alama 362 katika mtihani wa taifa na kuongoza
nchi nzima.
Alichofanya mwanafunzi Ejikeme Joy Mmeni ni kujiposti kwenye
mtandao akiwa na nakala ya matokeo ya kughushi akithibitisha kuwa yeye ndiye mwanafunzi
bora kitaifa.
Mmoja wa wafanyabiashara nchini humo aliiona posti hiyo na kuvutiwa
na matokeo hayo mazuri ambapo aliahidi kumfadhili masomo yake kwa gharama sawa na
dola 4,000 za Marekani.
0 Maoni