Zlatan Ibrahimovic atundika daluga rasmi

Mchezaji wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic, ameamua kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 41, na kumaliza zama zake za soko la kisasa lililompatia mafanikio.

"Ninasema kwaheri kwa soko, lakini si kwenu mashabiki," Mchezaji huyo raia wa Sweden aliwaambia mashabiki katika dimba la San Siro.

Ibrahimovic alishatangaza kwamba ataondoka katika klabu hiyo ya Italia, kabla ya jana kuaga katika mchezo wa mwisho wa ligi ya Serie A.

Mchezaji huyo amefunga magoli 511 kwa klabu, akiwa na Paris St-Germain, Manchester United na kwa AC na Inter Milan, na kutwaa ubingwa wa ligi kuu katika nchi nne.

Chapisha Maoni

0 Maoni