Afungwa kimakosa miaka 20 kwa kuwaua wanawe wanne

Mwanamke mmoja wa nchini Australia ambaye alipachikwa jina la "mwanamke mbaya muuaji wa mauaji ya mfululizo", ameachiwa huru baada ya ushahidi mpya kuonyesha hakuwaua watoto wake wanne wachanga.

Mwanamke huyo Kathleen Folbigg tayari ameshatumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa muaji ya watoto wake wa kiume Caleb na Patrick na mabinti zake Sarah na Laura.

Hata hivyo uchunguzi wa kisayansi uliofanyika katika siku za hivi karibuni, umebainisha kuwa watoto hao wote wanne, inaaminika walikufa kifo cha kawaida na wala hawakuuawa.

Kesi hiyo ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 55, imeelezewa kuwa ni moja ya kosa kubwa la utoaji haki, ambalo limefananishwa na haki iliyoharibiwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni