Rais Samia atoa neno sakata la Feisal na Yanga


 Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Klabu ya Yanga kumaliza mgogoro na kiungo Feisal Salum baada ya timu hiyo kupata sifa nyingi katika soka.


Rais Samia ametoa agizo hilo leo June 5, 2023 katika hafla ya chakula ya jioni ya kuwapongeza Yanga kwa kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika juzi Juni 3,2023 dhidi ya US Alger ya Algeria.


Haipendezi klabu kubwa kama hii kuwa na ugomvi na mtoto mdogo,  hebu kamalizeni,  kisha mje nyumbani kunieleza.” Amesema


Yanga wamekuwa na mgogoro wa kimkataba wa muda mrefu na kiungo huyo humu Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ambayo ilisikiliza malalamiko ya pande zote na kuamua kuwa mchezaji huyo bado anamkataba na Yanga mpaka 2024.


Kwa upande mwingine wakati akiipongeza timu hiyo amesema Yanga imeitoa kimasomaso Tanzania kwa hatua iliyofikia kwenye mashindano hayo.


“Nawapongeza mmekuwa nafasi ya pili na kama walivyosema ni mambo ya kikanuni vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine, mmetutoa kimasomaso hongereni sana, mafanikio haya hayakuja kwa kubahatisha ni matokeo ya jitihada za Wachezaji, Kocha na Viongozi wa Timu na Kamati tendaji”


“Shukrani ziende pia kwa Karia na Mtunza kapu la magoli Gerson Msigwa nimshukuru kwamba fedha yote iliyokuwa inatolewa alikuwa anaitoa kwa wakati, namshukuru pia Matindi Mkurugenzi Mkuu wa ATCL tulipomtaka atoe ndege aliitoa kwa wakati ingawa ameniletea invoice ya kulipa lakini ile kukubali ndege iende namshukuru”



Chapisha Maoni

0 Maoni