Yanga kujenga uwanja wa kisasa Jangwani, waomba eneo zaidi

 

Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said amesema kuwa klabu hiyo yenye maskani yake kwenye eneo la Jangwani mkoani Dar es Salaam, inampango wa kujenga uwanja wa kisasa katika eneo hilo.

Akiongea leo Ikulu, Dar es Salaam, wakati wa hafla ya mlo wa usiku walioandaliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwapongeza kwa kuwa washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika, Eng. Hersi amesema lengo ni kuunga mkono mipango ya nchi kuwa mwenyeji wa AFCON 2027.

"Mheshimiwa Rais Yanga inaeneo la Jangwani ambalo linahistoria kubwa Wazee wetu Mzee Abeid Amani Karume alishiriki kupatikana kwa ardhi na kujenga jengo letu la klabu," alisema Eng. Hersi na kuongeza "Lakini pia pembeni yake kunauwanja wa Kaunda ambao unahistoria ya Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda".

Amesema kwamba wao kama viongozi vijana wanataka kujenga uwanja katika eneo la Jangwani na wameshafanya 'feasibility study' eneo linafaa kwa kujenga uwanja ila kunamapunfugu ya ardhi.

"Mheshimiwa Rais pale Jangwani kuna eneo la ardhi ambalo serikali haijalipangia matumizi, kama tutapatiwa eneo lile tunaweza kujenga 'the state of the art stadium, ili nasi tuwe sehemu ya kusaidia AFCON 2027," alisema Eng. Hersi.

Chapisha Maoni

0 Maoni