Wajawazito wajifungua kwa mwanga wa tochi, huku milio ya risasi ikitawala

 

Wajawazito wanalazimika kujifungua hospitalini kwa kusaidiwa na mwanga wa tochi za simu kutokana na kukosekana kwa umeme katika hospitali chache ambazo bado zinatoa huduma, nchini Sudani.

Kama hilo halitoshi, milio ya silaha nzito huwa ikisikika katika hospitali hizo na kuwafanya wajawazito kujifungua watoto ambao wanachosikia kwanza ni milio ya silaha.

Mmoja wa madaktari Dk. Howaida Ahmed al-Hassan amesema kwamba wamekuwa wakitumia mwanga wa tochi za simu wakati wa kuzalisha kwa kutumia upasuaji.

Katika video aliyotuma watumishi wa afya ambao wote ni wanawake, wanaonekana wakimzunguka Dk. Hassan wakishika simu zao kummulikia akifanya upasuaji.

Chapisha Maoni

0 Maoni