Rais Samia aipongeza Yanga, awaalika mlo wa usiku Ikulu kesho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Yanga kwa kuhitimisha salama mchezo wake wa fainali ya Kombe la Shirikisho na kuandika historia ya mafanikio.

Kupitia akaunti yake ya twita Rais ameandika, "Historia mliyoiandika katika safari yenu ya michuano hii ni kubwa na ya heshima kwa Taifa letu. Nawatakia kheri katika mipango yenu ya siku zijazo"

.

Aidha, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaalika viongozi, wachezaji na banchi la ufundi la Yanga kesho Ikulu ya Dar es Salaam, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Swerikali Bw. Gerson Msingwa.



Chapisha Maoni

0 Maoni