Wagonjwa wa changamoto ya kupumua waongezeka Kenya

Kenya kwa sasa inaonekana kuwa inakabiliana na ongezeko la wagonjwa wanaohitaji oksijeni, wakati taifa hilo likikabiliwa na wimbi jipya la ugonjwa wa Covid-19.

Katika siku za hivi karibuni, idadi ya watu Kenya wanaobainika kuwa na virusi vya ugonjwa huo imeongezeka, wengi wakiwa na changamoto ya kupumua, inayohitaji msaada wa oksijeni. 

Wakati Wizara ya Afya haitoi tena taarifa za idadi ya wagonjwa wa Covid-19, haijulikana ni watu wangapi wamepata maambukizi, jambo ambalo ni muhimu ili watu wachukue tahadhari.

Huko China, kwa sasa wanakabiliwa na wimbi jipya la corona, ambalo linatarajiwa kusababisha maambukizi ya watu milioni 65 kwa wiki katika mwezi Juni.

CHANZO: Nation 

Chapisha Maoni

0 Maoni