Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Berlusconi afariki dunia

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi, bilionea na mmiliki wa vyombo vya habari, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.

Berlusconi ambaye wakati wa uhai wake alikabiliwa na kashfa za ngono, amefariki dunia katika hospitali ya San Raffaele Jijini Milan.

Mwezi Aprili, Berlusconi alitibiwa maambukizi ya kwenye mapafu yenyemahusiano na lukemia sugu.

Berlusconi kwa mara ya kwanza aliingia madarakani mwaka 1994 na kuongoza serikali nne hadi mwaka 2011.


Chapisha Maoni

0 Maoni