Ukraine yakomboa vijiji vitatu kutoka kwa Urusi

Ukraine imesema imevikomboa vijiji vitatu kusini mashariki na kusema ni makazi ya kwanza kukombolewa kutoka kwa Urusi, tangu Kyiv waanzishe mashambulizi.

Picha za video zinaonyesha vikosi vya Ukraine, vikishangilia huko Blahodatne na Neskuchne, na waziri wa ulinzi amesema wametwaa pia eneo karibu na Makarivka.

Ukraine kutwaa vijiji hivyo vitatu ni hatua kubwa ya kusonga mbele kukabiliana na uvamizi wa Urusi katika maeneo yanayoshikiliwa.

Hata hivyo Urusi bado haijathibitisha vikosi vyake kurejeshwa nyuma, badala yake imesema inakabiliana na mashambulizi ya Ukraine katika mkoa huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni