Balozi aliyewafananisha Waafrika na nyani aitwa kwao

Nchi ya Romania imemuita nyumbani balozi wake nchini Kenya, na kuomba radhi baada ya balozi huyo kuwafananisha Waafrika na nyani.

Balozi Dragos Tigau, alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano kwenye jengo la Umoja wa Mataifa, Jijini Nairobi Aprili 26, mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Tigau alisema "kundi la Waafrika limejiunga nasi" wakati alipoona nyani nje ya dirisha.

Kitendo hicho cha Balozi Tigau, kiliibuliwa hadharani siku ya Alhamsi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Kamau Macharia.

Chapisha Maoni

0 Maoni