Manchester City watwaa ubingwa wa UEFA

Timu ya Manchester City hatimae imefanikiwa kuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuifunga Inter Milan 1-0 huko Istambul, na kufanikiwa kutwaa mataji matatu katika msimu huu.

Baada ya kushinda Ligi Kuu ya Uingereza na Kombe la FA, City imefuata nyayo za Manchester United kutwaa makombe matatu mwaka 1999, na kuwa timu pekee za Uingereza kufanya hivyo.

Kikosi cha Kocha Pep Guardiola, hakikuwa katika kiwango chao bora dhidi ya Inter Milan waliokuwa wakicheza kwa uerevu, na kilijikuta kikipata pigo la kumpoteza Kevin de Bruyne kwa kuumia kipindi cha kwanza. 

Hata hivyo, mashabiki wengi wa Manchester City ndani ya dimba la Ataturk, hawakujali kuhusiana na hilo, wakati wakisherehekea kwa furaha usiku wa aina yake na msimu wa kihistoria wa klabu hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni