Vibaka wa bidhaa madukani wageuka janga la taifa Uingereza

 

Maduka makubwa ya bidhaa ya Uingereza yameaza kuweka alama za usalama kwenye mapande ya nyama na jibini katika kukabiliana na wimbi la wizi unaofanywa na wateja wasio waaminifu.

Baadhi ya maduka yamechukua hatua zaidi ya kuweka idadi chache ya bidhaa hizo kwenye mashubaka, katika jitihada za kupunguza wizi.

Hii inafuatia kutolewa kwa takwimu na shirika la BBC, zinazoonyesha kwamba sasa wizi wa bidhaa madukani umekuwa ni janga, kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Wamiliki wa maduka ya bidhaa wamesema kwamba wamelazimika kutumia fedha nyingi katika kuimarisha ulinzi.

Mwezi Machi, vikosi vya polisi vay England, Wales na Kaskazini Ireland walitoa rekodi ya matukio  33,000 ya vibaka waliiba bidhaa madukani.

Chapisha Maoni

0 Maoni