Mbio za kuwania urais wa Marekani 2024, kwa tiketi ya chama cha
Republican zinakaribia kupanda joto, kufuatia vigogo wawili zaidi kutarajiwa
kuingia kwenye kinyang’anyiro.
Aliyekuwa Makamu wa Rais Mike Pence na aliyekuwa Gavana na
News Jersey Chris Christie wanajiandaa wiki ijayo kuingia ulingoni.
Wagombea hao wanatarajia kutoa upinzani wa aina yake kwa kwa
aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump.
Hatimaye mshindi wa upande wa Republican anatarajiwa
kuchuana na Rais Joe Biden, wa Democrat, katika uchaguzi wa Novemba mwakani.
0 Maoni