Matola aja kivingine Simba


 Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba  imemteua  ya Selemani Matola kuwa Kocha Mkuu wa timu za vijana. 

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Imani Kajula amesema Simba imedhamiria kuboresha programu za vijana ikiwa ni muendelezo walichokuwa wakikifanya miaka 11 iliyopita.


“Simba inaamini kwa dhati kabisa ili kuwa na timu imara ni lazima tuwe na timu imara za vijana, kama ilivyomtoa Jonas Mkude na Hamis Ndemla waliotoka kwenye programu za vijana.” Imani Kajula.


Kwa upande wake kocha mkuu wa program hiyo ya vijana Seleman Matola amesema imekuja kwenye wakati sahihi,“Sintaiangusha bodi sintaiangusha klabu ya Simba.” Selemani Matola

Simba wanalenga kuwa na timu bora ya baadae kupitia uwekezaji wa kwenye soka la Vijana ambapo wanaenda na kauli mbiu isemayo wakati ujao ni sasa.


Kocha Suleiman Matola kwa sasa amehitimu masomo yake ngazi ya Daraja A baada ya kukamilisha madaraja B na C akiwa ndani ya timu hiyo akitumikia kama kocha msaidizi.


Katika kuboresha program ya vijana timu hiyo imemteua  meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu kuwa mkuu wa programu.


Rweyemamu amesema ili mpira uweze kuendelea ni lazima kuimarisha timu za vijana

“Takribani wachezaji 250 tumewakuza katika programu za vijana na naweza kusema hakuna timu yoyote nchini katika ngazi zote ambayo haijanufaika na mchezaji kutoka kwenye timu za vijana za Simba” Patrick Rweyemamu.


Mwaka 2008-2015 Simba kupitia programu hiyo waliweza kufanikiwa kuzalisha wachezaji vijana ambao mpaka sasa wanafanya vizuri katika ulimwengu wa soka. Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Sesemi ni miongoni mwa zao la mradi huo.


Chapisha Maoni

0 Maoni