Rais Dk Mwinyi azindua kamati ya maridhiano Zanzibar

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi ameonesha dhamira ya maridhiano na kukutana  viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuendeleza dhamira ya kushirikiana na kuimarisha Umoja wa Kitaifa Zanzibar.


Dk Mwinyi amezindua kamati hiyo  Mei 31, 2023 Ikulu, Zanzibar na kumshukuru Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM kuridhia, kufanya vikao na viongozi wa vyama vya siasa.


Lengo kusikiliza maoni yao ambayo ameendelea kuyafanyia kazi na kutekeleza kwa vitendo azma ya kuleta maridhiano ya kisiasa ikiwemo kuunda Kikosi Kazi kilichopitia ripoti ya mkutano wa Baraza la vyama vya siasa na kutoa mapendekezo.


Vilevile kwa kuimarisha uhuru wa kisiasa na kidemokrasia kwa kuruhusu tena mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kuanzisha mchakato wa katiba mpya.


Dk Mwinyi amesema hotuba yake aliyoitoa mwezi Novemba mwaka 2020 alipozindua Baraza la Wawakilishi kuwa dhamira yake ni kuwaunganisha wananchi wote wa Zanzibar kuwa wamoja, bila kujali rangi, asili, imani za dini au itikadi za kisiasa.


Halfa hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Othman Masoud Othman na ujumbe wake pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Hemed Suleiman Abdullah na ujumbe wake.

Chapisha Maoni

0 Maoni