UKALI WA MAISHA: Vigogo Kenya kuongezewa mishahara

 

Maafisa wa Ikulu, akiwamo Rais na Naibu Rais, Mawaziri na Wabunge, wanatarajiwa kupatiwa nyongeza ya mishahara ya asilimia 14 katika kipindi cha miaka miwili ijayo, kuanzia mwezi ujao, kufuatia mapendekezo ya Tume ya Miashahara na Maslahi (SRC) ili kupunguza makali ya kupanda kwa gharama za maisha.

Iwapo mapendekezo hayo yataridhiwa, maafisa hao watapata ahueni kubwa kutokana na madhara ya kuendelea kuwapo kwa mfumuko mkubwa wa bei, ambao umekuwa ukiathiri vipato vyao kutokana na gharama za bidhaa za mahitaji ya msingi.

CHANZO: Nation



Chapisha Maoni

0 Maoni