Mbappe ataka kumalizwa ghasia nchini Ufaransa

 


Kapteni wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe, ametaka ghasia nchini humo kukomeshwa, kufuatia kifo cha dereva kijana aliyeuawa na polisi.

Ufaransa imeshuhudia machafuko baada ya kijana huyo Nahel M (17) kupigwa risasi na kufa akikaidi kusimama kwenye kizuizi, Jumanne.

“Ghasia hazitatui kitu, hususani zikiwa zimewageukia wale ambao wanaoonyesha hasira zao,” ameandika Mbappe kwenye Instagram yake.

Mchezaji huyo wa soka wa timu ya PSG na timu ya Taifa ya Uingereza, mwenye umri wa miaka 24, ameshauri kuwapo kwa maandamano ya amani na yenye kujenga.

Chapisha Maoni

0 Maoni