Ghasia na uporaji vitu madukani vyapamba moto Ufaransa

 

Vitendo vya ghasia na uporaji wa vitu madukani vimeshika kasi nchini Ufaransa, kufuatia polisi kumuua kwa risasi dereva kijana Nahel M, aliyepita na gari eneo la kusimama.


Wakati ghasia hizo zilizoambatana na kuchoma moto magari zikiendelea imeibuka picha ya rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron akiponda raha na mwanamuziki Elton John, hali iliyoibua hasira zaidi.

Watu wapatao 667 wamekamatwa, wakati mapigano baina ya waandamanaji na polisi nchini Ufaransa yakiendelea kwa siku ya tatu mfululizo katika maeneo mbalimbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni