Rais Samia ataja sababu za kuwateua Lukuvi na wenzake

Rais Samia Suluhu Hassan amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua na kuwapa ujumbe wa utendaji kazi katika kila eneo alilopangiwa.


Akizungumza baada ya kuwaapisha Rais Samia ametaja sababu za kuwateua  viongozi wanne akiwemo WIlliam Lukuvi, Abdalah Bulembo , Haji Omar, Balozo Rajab Luhwavi amesema tunakokwenda kuna kazi kubwa ya kuoanisha siasa na maendeleo yetu ya jamii 


Amesema siasa tumeiachia chama completely lakini kule kwenye chama kuna nenda rudi vuta nikuvute  nilimteua Mkuchika kuwa Waziri mwenye kazi maalumu hii ndiyo kazi maalumu” 


“Peke yake asingeweza kufanya kwahiyo nimemteulia mavererani  wenzie hawa waende wazame huko chini watuambie nini kinakosekana jamii ikoje na siasa na siasa zetu nchini zinaendaje mambo yakoje waende wakatutafutie huko na waje na mapendekezo nini tufanye”




Chapisha Maoni

0 Maoni