Adolf Mbinga kuzikwa Nachingwea Lindi

 

Mwanamziki Bendi ya Sikinde OG, Adolph Nicholas Mbinga Kuzikwa kesho Juni 17 Nachingwea.


Akithibitisha kuhusu maziko ya mwanamuziki huyo aliyefariki  dunia usiku wa Alhamis Juni 15 Asha Baraka ambaye ni mmiliki wa bendi ya Twanga pepeta amesema Marehemu aliyekuwa akiishi Tabata alisafirishwa nyumbani kwao Nachingwea kupumzika na ndipo umauti ulipomfika.


Amesema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu wa familia ni kwamba anatarajiwa kuzikwa kesho huko kijijini kwao Mpute  katika wilaya ya  Nachingwea mkoani Lindi.


Marehemu Mbinga aliyekuwa mpiga solo mahiri na alikuwa  mmoja wa waasisi wa Bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' na aliwahi kupitia katika bendi mbalimbali kama vile Diamond Sound, Mchinga Sound na Mlimani Park 'Sikinde'.

Chapisha Maoni

0 Maoni