Papa Francis kufanyiwa upasuaji tumboni

Papa Francis atafanyiwa upasuaji tumboni jumatano mchana katika hospitali ya Gemelli iliyopo Jijini Rome.

Vatican imesema Papa anatarajiwa kukaa hospitali kwa siku kadhaa, ili kupona baada ya kufanyiwa upasuaji wa henia.

Henia imekuwa ikimsababishia maumivu yanayojirudia na dalili mbaya, ameeleza Msemaji wa Vatican Matteo Bruni.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani mwenye umri wa miaka 86, amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni.

Chapisha Maoni

0 Maoni