Mabehewa ya ghorofa yaanza kuwasili Dar

Mabehewa 6 sita ya ghorofa kati ya 30 yaliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kutoka nchini Ujerumani yameanza kuwasili hapa nchini.  

Mabehewa hayo ya ghorofa yameanza kushushwa leo katika bandari ya Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema mabehewa hayo yana uwezo wa kubeba abiria 140 kwa daraja la 3 na abiria 123 kwa daraja la pili.  

Mabehewa mengine 24 pamoja na vichwa vya abiria yanatarajiwa kuendelea kuwasili nchini kwa nyakati tofauti kuanzia mwezi ujao.  

Wiki iliyopita Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema mabehewa na vichwa vya treni vimechelewa kufika nchini kutokana na watengenezaji kuchelewa kukamilisha matengenezo kulikosababishwa na changamoto ya upatikanaji wa vipuri.

CHANZO: MAELEZO 

Chapisha Maoni

0 Maoni