Makombora ya Urusi yawaua mapacha hawa

 

Mashambulizi ya makombora ya Urusi yamewaua mapacha wakike katika eneo la kati la Kramatorsk mashariki mwa Ukraine kwenye mkoa wa Donetsk.

Mapacha hao ambao ni miongoni mwa watu kumi waliouawa katika mashambulizi hayo wametajwa kuwa ni Yuliya na Anna Aksenchenko wenye umri wa miaka 14.

Eneo la Kramatorsk linamilikiwa na Ukraine, lakini lipo karibu eneo la nchi hiyo linalokaliwa kimabavu na wanajeshi wa Urusi.


Chapisha Maoni

0 Maoni