Wakazi wa Kijiji cha Magata Kata ya Karutanga mkoani Kagera wamejawa na simanzi baada ya watoto wawili wa familia moja kufa baada ya kufunikwa na kupondwa mawe wakati wakichimba mchanga katika eneo la Marahara.
Diwani wa Karutanga,
Alhaji Yakubu Mahamoud, amewataja watoto waliokufa kuwa ni Samsoni Eliud (13) na Emmanuel Eliud (10) ambao
wote walikuwa ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Magata.
Diwani Mahamoud
amesema kuwa watoto hao waliokuwa
wakilelelewa na mama yao walipotea Juni
26 mwaka huu na walitafutwa katika maeneo yote hawakuweza kupatikana na Juni 27
watoto hao ndipo walipopatikana wakiwa tayari wamekufa baada ya kufukiwa na mawe wakati wakichimba mchanga.
Kufuatia
tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga alifika katika eneo
hilo na kupiga marufuku na kuzuia mtu yeyote kufanya shughuli za uchimbaji wa
mchanga kwa kuwa eneo hilo sio salama na kuagiza kukaguliwa maeneo yote ya
uchimbaji wa mchanga katika wilaya hiyo ili kudhibiti maafa kama hayo kutokea.
0 Maoni