Mabaga Fresh walivyomsogeza Juma Nature kwa Majani

Kundi la muziki la kitambo la Mabaga fresh lenye maskani yao Temeke Dar es Salaam ndiyo waliomtambulisha Juma Nature kwa P Funk Majani.

Akinyetisha ukweli huo mmoja wa wanakundi wa Mabaga fresh Dj Snoxx amesema ilikuwa mwaka 1999 ambapo wakisuka wimbo ulifahamika kwa jina "Mtulize" ndipo walimshirikisha Juma Nature maarufu kama kiroboto enzi hizo akiwa anasoma kidato cha pili sekondari ya Cekafa huko Tandika.


Kwa mujibu wa mnyetishaji huyo anasema walipomchukua Nature kwa mtayarishaji wa muziki P Funky Majani ambaye ndiye aliyemaliza mchongo mzima wa wimbo wa "Mitulize" alitamani sana kufanya kazi na Juma maana aligundua uwezo wake.


Anaeleeza kuwa enzi hizo Nature alikuwa kwenye kundi lake la FGM na mchakato wa kudondosha wino chini ya Majani haukuwa mgumu japo kulikuwa na mvutano kati ya Majani na Marehemu Ruge ambaye alikuwa anamiliki lebo ya Smooth Vibes akiwa na hamu na kumsaini Nature matunda yaliyozaa kolabo la Lady Jaydee na Nature.



Baadae Juma kiroboto akakubali kuwa chini ya Majani kwani enzi hizo alikuwa ni mtayarishaji mwenye umiliki wa mitambo yote muhimu ya upishi wa muziki mpaka kumfikia mteja.

Chanzo:Ufm




Chapisha Maoni

0 Maoni