Mourinho ni muda tu kabla ya kuchukuliwa hatua na UEFA

UEFA inangojea ripoti ya maafisa wa mechi na wajumbe wake, kabla ya kufanya uamuzi wa kumchukulia hatua kocha wa Roma Jose Mourinho, kwa kumtolea lugha chafu refa Anthony Taylor katika fainali ya Europa.

Mourinho alimkosoa refa Taylor kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, baada ya Roma kushindwa kutwaa ubingwa wa Roma, kwa kufungwa na Sevilla kwa mikwaju ya penati 4-1 katika fainali iliyochezwa Budapest.

Baadae kocha huyo machachari alinaswa kwenye kamera akiwa katika eneo la kuegeshea magari akibwatuka maneno machafu, huku akimnyooshea kidole refa Taylor na maafisa wengine waliokuwa wakipanda basi dogo.

Katika mchezo huo uliogubikwa na hasira, Mourinho alipewa kadi, huku refa Taylor akirejea mara kwa mara kuyataka mabenchi ya timu hizo kuchukua hatua, huku refa msaidizi Michael Oliver akipata wakati mgumu kuumudu mchezo.

Refa Taylor alitoa kadi za njano 13 kwa wachezaji, ambapo ni idadi kubwa ya kadi kutolewa katika ligi ya Europa. Kadi saba zilizotolewa walipewa wachezaji wa Roma, ikiwa ni rekodi kubwa kwa mchezo wa fainali.

Kocha wa Roma Jose Mourinho akiirushwa kwa mashabiki medali ya mshindi wa pili wa Ligi ya Europa aliyopewa kutokana na kukerwa na matokeo ya kushindwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni