Rais Museveni ajibu mapigo msimamo ushoga


 Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameweka msimamo wa nchi hiyo kuhusu ushoga na kuyatahadharisha mataifa ya Magharibi yaliyotishia kuiwekea nchi hiyo vikwazo.


Museveni amesema ikiwa mataifa hayo yatawanyima misaada kutokana na kupitisha sheria ya kupinga ushoga basi watakaa chini na kupunguza matumizi ya nchi kwa kubana matumizi huku wakipanga bajeti kwa umakini lakini kamwe hawatoifuta sheria kwa kuogopa vikwazo vya Mataifa ya magharibi.


Museveni ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na Wanachama wa Chama cha NRM katika kile kinachoonekana ni kama anamjibu Rais wa Marekani Joe Biden aliyetishia kuiwekea vikwazo Uganda baada ya kupitisha sheria hiyo.


Museveni amesema “Kuhusu biashara wakituingilia kwenye biashara zetu, tutafanya biashara na Watu wengine, hakuna Mtu atakayetubabaisha wala kututingisha, Waganda mnapaswa kuwa tayari kwa vita, vita ni ya Majasiri sio kwa Watu Wadhaifu”


Amesema Chama hicho hakijawahi kutumia lugha mbili tofauti na kwamba wanachokisema mchana ndicho watakisema usiku “Zoezi la utiaji saini wa muswada umekamilika, hakuna Mtu atakayetubabaisha wala kututingisha, Waganda mnapaswa kuwa tayari kwa vita, vita ni ya Majasiri sio kwa Watu Wadhaifu”


Katika sheria hiyo mtu yeyote anayesambaza ushoga anaweza kuhukumiwa kwa kifungo cha kifo ambapo amesema sheria imeshapita na haiwezi kufutwa, Sheria hiyo mpya itawalazimu Watu wanaoshiriki kwenye vitendo vya ushoga kutumikia hadi kifungo cha maisha jela.

Chapisha Maoni

0 Maoni