Ajali ya treni tatu yaua watu 238 na kujeruhi 600 India

 

Watu wapatao 238 wamekufa na wengine 650 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha treni tatu katika jimbo la mashariki la Odisha nchini India.

Mmoja ya treni ya abiria iliacha njia na mabehewa yake kuangukia kwenye njia ya pili ya treni ambayo kulikuwa na treni inayopita.

Shirika la Reli la India limesema treni zilizohusika kwenye ajali hiyo mbili ni za Coromandel Express na moja ni ya Howrah Superfast Express.

Maafisa wa nchini India wamesema kwamba ajali hiyo ni mbaya kuwahi kutokea katika karne hii.

Chapisha Maoni

0 Maoni