Neema Swai kinara ujio ndege ya mizigo yenye uwezo kubeba tani 54

 

Ndege  ya kwanza ya mizigo ikiwa imewasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, nakupewa makaribisho rasmi ya kumwagiwa maji.



Ndege hiyo imeongozwa na marubani watatu akiwemo Rubani Mtanzania, Neema Swai wa  Shirika la Ndege nchini Air Tanzania ndiye aliyeirusha  Ndege Mpya ya Mizigo aina ya BOEING 767-300F kutoka nchini Marekani mpaka uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport jijini Dar es Salaam


Kimuundo Matanki yake ya mafuta yana uwezo kubeba lita 90,770, mabawa yake yana urefu wa meta 47.6, pia inaweza kwenda mwendokasi wa kilometa 850 kwa saa na ina urefu wa meta 54.9.



Ndege hiyo imetajwa kufungua fursa ya Masoko kimataifa wakati  itakapokuwa ikitoa huduma ya usafirishaji wa mizigo kwa Tanzania na Afrika Mashariki. Ikitoa utatuzi wa changamoto za usafirishaji wa mizigo kwa Wafanyabiashara nchini kwa kusafirisha kwa gharama nafuu na kwa urahisi.


Ndege hii ina uwezo wa kubeba tani 54 za mzigo , ina uwezo wa kusafiri kilometa 11,070 za angani bila kutua kuongeza mafuta sawa na  muda wa saa 10 bila kutua.

Chapisha Maoni

0 Maoni