THBUB yamaliza utata kifo cha mwanafunzi UDOM


 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa matokeo ya uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Nusura Abdallah.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, amesema  kifo hicho hakikuwa na uhusiano wowote na ajali ya Naibu Waziri Dk Festo Dugange iliyotokea Aprili 25 kuamkia 26 mwaka huu.


Katika taarifa yake Jaji Mwaimu amesema walitembelea mikoa ya Dodoma, Singida na Kilimanjaro na kwamba matokeo yanaonyesha kuwa kifo cha Nusura kilisababishwa na shambulio kali la kupanda kwa sukari na upungufu wa damu.

Kwa mujibu wa Tume safari ya Nusura kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro ilianza Aprili 27, 2023 kwa basi la Manning Nice baada ya gari la Kapricon alilopanga kusafiria awali kuchelewa. Hata hivyo basi hilo lilimfikisha Babati na baadaye alipanda Coaster hadi Arusha, kisha kumalizia safari yake hadi Moshi kwa basi la Ibra Line.

https://mimihabari.blogspot.com/2023/05/udom-yafichua-siri-utata-wa-kifo-cha.html

Baada ya kufika saa tano usiku, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Nusura alipokelewa na mchumba wake, Juma Mohamed Kundya mjini Moshi hadi nyumbani.

“Lengo la safari hiyo lilikuwa ni kuzungumzia masuala ya uchumba wao na kupanga siku ya kwenda kujitambulisha nyumbani kwao Singida. Aidha, alipanga kukaa hapo hadi Mei 2, 2023 ndipo arejee Dodoma,”


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, wamegundua kuwa Mei mosi mwaka huu marehemu aliandaa chakula cha jioni nyumbani kwa mpenzi wake Juma Kundya mjini Moshi; ambacho alikula yeye, mchumba wake na mpwa wa mchumba wake.


Hata hivyo baada ya kumaliza kula, marehemu Nusura alijisikia vibaya na kuanza kutapika hadi kuishiwa nguvu, hali iliyosababisha kufikishwa Hospitali ya Faraja kwa matibabu na hadi umauti ulipomfika


Uchunguzi wa tume hiyo umebaini, Nusura aliwasiliana kwa mara ya mwisho na familia yake, Aprili 29, 2023 na Mei 1, 2023 ilikuwa mara ya mwisho kuwasiliana na rafiki anayesoma naye chuoni.

Chapisha Maoni

0 Maoni