UDOM yafichua siri utata wa kifo cha Nusura Abdalah

 

Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kimejitokeza hadharani na kutoa taarifa kuhusu kifo chenye utata cha mwanafunzi Nusura Hassan Abdallah.


Katika taarifa yake iliyotolewa na kitengo cha masoko na mawasiliano UDOM imeeleza kuwa katika mitandao ya kijamii kumekuwepo na taarifa ambayo siyo rasmi kuhusu kifo cha mwanafunzi huyo.


Taarifa hiyo imefafanua kuwa Nusura Hassan alikuwa ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza  ya sayansi ya elimu na kuwa hadi kufikia tarehe 27/04/2023 marehemu alionekana shuleni akiendelea na masomo.


Tarehe 3/5/2023 uongozi wa chuo ulipokea taarifa kutoka kwa mwanafunzi ambaye alikuwa anasoma naye kuwa amepokea taarifa kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni mjomba wa marehemu kuwa amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Faraja iliyopo Himo Kilimanjaro.


Imefafanua zaidi na kusema uongozi baada ya taarifa hiyo uliwasiliana na dada yake anayeishi Uchira ambaye alithibitisha kutokea kwa kifo cha mdogo wake, na mwili wa marehemu ulisafirishwa nyumbani kwao Iramba mkoani Singida.

Baada ya kujiridhisha uongozi ulifanya taratibu zote za pole kwa familia  na mazishi ya Nusura yalifanyika tarehe 4/05/2023 Iramba.

MTANDAONI KWAFUKUTA

Kabla ya kutolewa taarifa rasmi na uongozi wa UDOM katika mitandao ya kijamii haswa mtandao wa twita wadau walikuwa na maoni mengi kuhusu utata wa kifo hicho kikihusishwa na kigogo wa serikali.


Chapisha Maoni

0 Maoni